Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Samia Suluhu Hassan ametuma salamu za rambirambi kwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Queen Sendinga kutokana na vifo vya Watu 19 katika ajali iliyotokea alfajiri leo June 10, 2022.
Ajali hiyo imetokea alfajiri ya tarehe June, 2022 katika Wilaya ya Mufindi Mkoani Iringa na kusababisha vifo vya Wanaume 14, Wanawake 4 na mtoto mmoja wa kike.
Kwa Mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoani wa Iringa, ACP Allan Bukumbi, basi dogo la abiria aina ya Coaster lililokuwa likisafiri kutoka jijini Dar es Salaam kwenda Iringa liligonga lori lililokua limeharibika katika eneo hilo.