Club ya Man City imemtambulisha rasmi Erling Haaland (21) kutokea Borussia Dortmund kwa mkataba wa miaka mitano sasa atakuwa Etihad hadi 2027.
Haaland atajiunga na Man City kuanzia July 1 kuelekea maandalizi ya msimu mpya wa Ligi Kuu England na mashindano mbalimbali.
Kinda huyo raia wa Norway ambaye anafuata nyayo za baba yake aliyewahi kucheza Man City, hadi anajiunga na Man City amecheza jumla ya mechi 21 timu ya Taifa na michezo 89 ya club akiwa na Borussia Dortmund na kufunga magoli 86.