Rais Samia Suluhu Hassan amesema Mtu yeyote mwenye akili ya kawaida anaweza kuwa mwepesi kutoelewa safari anazofanya nje ya Nchi na kubaki kulaumu “Rais anasafiri tu”
Rais amesema haya Ikulu Dar es salaam wakati wa hafla ya utiaji saini mkataba wa ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) sehemu ya Tabora hadi Isaka, KM 165 njia kuu na KM 35 njia za kupishana.
“Gharama za ujenzi wa mkataba huu ambao leo tumesaini ni dola za Kimarekani karibu milioni 900 ambazo ni sawa na zaidi ya Tsh. Trilioni 2 lakini DSM – Mwanza ni zaidi ya Tsh. Trilioni 16, niliposema tutatejanga vipande vyote sikujua pesa natoa wapi lakini kwasababu ya kufunguka, kufuata Watu kuita Watu tuzungumze pesa imepatikana”
“Tunakwenda kuanza awamu ya pili mpaka Kigoma kule tukaungane na wenzetu…………… tupo kwenye mazungumzo ya jinsi ya kuzipata fedha za awamu ya pili, tunapoita Watu hapa ndani tukazungumza, tunapowafuata walipo kwenda kuzungumza matokeo yake ndio haya, wale wenye akili za kawaida ni rahisi kulaumu ‘Rais anasafiri tu, Rais hakai, badala ya kutembelea Mikoa anatembelea tu nje’ lakini matokeo yake ndio haya”
“Nikienda Mikoani nitajenga siasa ya ndani hakuna maendeleo, nikienda nje nakwenda kutafuta fedha hizi kwa ajili ya maendeleo……. sio kazi rahisi ndani ya mwaka mmoja na miezi michache ujenge vipande vyote hivi vya reli” ——— amesema Rais Samia.