Katika Shamrashamra za kuelekea kwenye Harusi ya Billnass na Nandy wawili hao leo July 12, 2022 walifika katika Kipindi cha Leo Tena kuzungumza mipango yao na mengineyo.
Billnass akizungumza katika kipindi hicho alieleza sababu za wao kufunga ndoa na kusema..’Wakati huu ni wakati sahihi wa kuwa pamoja na kufunga ndoa kuna wakati Billnass alishawahi kuni surprise pete Kwa kipindi kile alikuwa tayari yeye kuingia kwenye ndoa lakini Kwa upande wangu sikuwa tayari. Na kwao aliambiwa sio sawa kuvishana pete wenyewe na pia kwetu niliambiwa sio sawa. kwahiyo tulijipa muda kama tunaweza kufunga ndoa. Kwa sasa hivi tumeweza na ni muda sahihi wa kufunga ndoa”- Billnass
Aidha Billnass alizungumza kuhusu ujio wa mtoto wao na kusema..”Huyu ni Mtoto wangu wa kwanza. Kuhusu jina bado hatujapanga unajua kuna watu wetu wametufanyia vitu vingi anaweza akaitwa jina la kizalendo akaitwa hata Shishi au Mchafu Chakoma au hata Steve”- Billnass
Na hizi ni baadhi ya picha kutoka kwenye mahojiano hayo yaliyofanyika Clouds FM.