Mahakama ya Wilaya ya Arusha imemhukumu kifungo cha maisha jela Fadhil Sumayani (30) ambaye alikuwa mlinzi kwenye nyumba ambayo haijaisha kwa kosa la kulawiti na kumbaka mtoto mwenye umri wa miaka tisa.
Tukio hilo ambalo linatajwa kufanyika September 19,2021 wakati mtoto huyo alipokuwa ametumwa na mama yake kwenda dukani kununua mahitaji ya nyumbani
Akitoa hukumu hiyo ya Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Wilaya ya Arusha Gwantwa Mwankuga amesema amemtia hatiani kwa kuwa upande wa mashtaka kupitia kwa mwendesha mashtaka wa Serikali Lilian Mmasi walileta mashahidi ambao walithibitisha tukio hilo pasipo kuacha shaka yeyote.