Rais wa Shirikisho la soka Duniani (FIFA) Gianni Infantino wakati wa mkutano wa 44 wa CAF ambapo Mgeni Rasmi akiwa Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa aliongea na waandishi wa habari na kuulizwa maswali kadhaa.
Infantino aliulizwa kuhusiana na Afrika kuwahi kuwa mwenyeji wa Kombe la Dunia mara moja tu (2010 Afrika Kusini) anatusaidiaje kuona Afrika inapata nafasi ya kuwa mwenyeji tena.
“Tupo hapa pia kwa ajili ya hilo tunataka Afrika iwe mwenyeji wa michuano mingi mikubwa ya kidunia kama alivyosema Motsepe”
“Hata AFCON sasa ni michuano mikubwa ya kidunia na ina wachezaji wakubwa wanaofanya vizuri katika vilabu bora duniani ni wachezaji wanaotokea Afrika”
Hata hivyo kwa upande wa Rais wa Shirikisho la soka Afrika (CAF) Patrice Motsepe amesema moja kati ya vitu watajadili ni pamoja na ombi la Tanzania la kutaka kuwa mwenyeji wa fainali za mataifa ya AFCON kwa kushirikiana na jirani yake Uganda.
“Kuna vitu muhimu tunaenda kujadili, kama nilivyosema tunaenda kujadili kuhusiana na Maendeleo ya soka lakini moja kati ya jambo kubwa ni kwamba Tanzania inataka kuwa mwenyeji wa AFCON wakishirikiana na Uganda, Kama unakuwa mwenyeji wa AFCON hii ni michuano mikubwa ya kidunia”>>> Motsepe