Tume ya uchaguzi na mipaka nchini Kenya(IEBC), imekamilisha mchakato wa uhakiki wa kura za urais
Macho yote sasa ni kwa Mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati wakimsubiri atangaze matokeo.
Wakati hayo yakijiri viongozi wa vyama vyote vya kisiasa walio katika ukumbi wa Bomas ambao ndio kituo kikuu cha kujumlisha kura wameonekana wakicheza nyimbo za dini, zinazotumbuizwa na kwaya katika ukumbi huo .
Tume ya uchaguzi inatarajiwa kumtangaza rais mteule leo.
Tume hiyo ina siku hadi saba za kutangaza matokeo baada ya uchaguzi kufanyika. Uchaguzi mkuu wa Kenya ulifanyika Jumanne wiki iliyopita tarehe 9 Agosti.
Iwapo mshindi wa urais atatangazwa leo,na iwapo hapatakuwa na pingamizi ya ushindi wake mshindi anafaa kuapishwa tarehe 30 mwezi huu wa Agosti.
Na hapa nakusogezea picha ushuhudie Mgombea Willima Ruto akiwasili katika Ukumbi wa Boma mahali ambapo matokeo ya Urais yanatarajia kutangazwa leo hii