Club ya KRC Genk ya Ubelgiji imetangaza rasmi kumrejesha nahodha wa Timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars Mbwana Samatta katika kikosi chao kwa mkataba wa mkopo wa mwaka mzima akitokea Fenerbahce ya Uturuki.
Samatta (29) ambaye anarejea KRC Genk baada ya kuondoka kwa miaka miwili, anarejea sehemu ambapo ufalme wake wa soka la Ulaya ndio ulianzia na anapendwa na kuheshimiwa na mashabiki wengi wa KRC Genk toka alipowasili kwa mara ya kwanza 2016 na kuondoka 2020 kujiunga na Aston Villa ya England.
Mbwana Samatta hadi anaondoka KRC Genk 2020 na kujiunga na Aston Villa alikuwa ameichezea KRC Genk michezo 191 na kufunga magoli 76, assist 20, huku akichangia kwa kiasi kikubwa KRC Genk kuchukua Ubingwa wa Ligi Kuu Ubelgiji msimu wa 2018/2019.