Mamlaka ya Uhifadhi Wanyamapori Tanzania Ikiongozwa na Kaimu Kamishna wa Uhifadhi Ndugu Mabula Nyanda wameitembelea ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro Mh. Fatma Mwasa kwa Lengo la kumsalimia, kujitambulisha na kumpa taarifa zinazohusu Uhifadhi katika Mkoa wa Morogoro.
Katika salamu hizo, Kamishna wa Uhifadhi alimpatia taarifa ya shughuli mbalimbali ambazo TAWA inayashughulikia hasa katika Pori Tengefu la Kilombero, Fursa na changamoto pamoja na hatua mbali mbali ambazo TAWA imeshachukua katika kukabiliana nazo.
Naye Mkuu wa Mkoa kwa upande wake ameishukuru TAWA kwa kufika ofisini kwake, kumkaribisha Morogoro, na kuonyesha ushirikiano katika masuala mbalimbali yanayohusu Maendeleo katika Mkoa wegu wa Morogoro.
ameelezea umuhimu mkubwa wa TAWA kwa mkoa wa Morogoro katika masuala ya Uhifadhi wa Vyanzo vya maji ambavyo vimekua vikiharibiwa kutokana na uvamizi wa mifugo, ukataji miti na uchomaji wa misitu.
“Uwepo wenu hapa mkoa wa Morogoro ni muhimu sana hasa ikizingatia watu zaidi ya milioni 11 wa Mkoa wa Morogoro na maeneo jirani wanategemea maji ambayo vyanzo vyake ni kutoka katika mkoa wa Morogoro na nitashangaa sana kama mtaharakisha kuhamia Dodoma wakati bado mkoa wa Morogoro unawahitaji sana. katika masuala ya uhifadhi ili kulinda vyanzo vya maji ambavyo bila jitihada kubwa kuchukuliwa vyanzo hivyo vitakauka” Alisema Mh. Fatma Mwasa.
Kamishna wa TAWA alimkabidhi Mkuu wa Mkoa Nembo ya TAWA na Jarida ambalo lina habari za TAWA.