Siva Moodley ana kundi la Wafuasi ndani na nje ya Afrika Kusini na anaheshimika miongoni mwa jumuiya ya kidini kwasababu ya ‘miujiza’ aliyoifanya wakati wa mahubiri yake pale alipokuwa hai.
Mitandao ya South Africa imeripoti kuwa tangu kifo chake karibia siku 400 zilizopita, Mchungaji Moodley amehifadhiwa kwenye nyumba ya kuhifadhia maiti iitwayo Martins Funeral Home, Taasisi hiyo, iliyoko Fourways, imelipwa ili kumweka Kiongozi huyo wa imani katika uangalizi wao lakini hata mtiririko wa pesa wa karibia R60 000 (Tsh. 8,137,595) uliotolewa kama bima ili kuhifadhi mwili huo unaanza kupungua.
Martin du Toit anayeendesha nyumba hiyo ya kuhifadhia maiti, hivi karibuni alisema anaomba idhini kutoka kwa Mahakama ili kuchoma mwili huo, huku ikionekana kuwa hata Wafusi wake wamekata tamaa juu ya ufufuo wake kwasababu mwili wake haujatembelewa na Mtu yeyote kwa zaidi ya miezi 12 sasa.
Inasemekana kuwa Mzer huyo wa miaka 53, ambae alikuwa Mwanzilishi wa Kaniaa la ‘The Miracle Centre’ lililoko kaskazini mwa jiji la Johannesburg alifariki dunia tarehe 15 Agosti mwaka jana baada ya kuugua, Kanisa lake halijakiri kifo chake kwenye mitandao yao ya kijamii mpaka leo, na akaunti zake za Twitter bado zipo active na kujibu Watu kama vile ni yeye.