Ni Headlines za Shirika la Mpira wa Kikapu (NBA) linalosimamia mpira wa kikapu nchini Marekani na Canada ambapo time hii wameungana na MMI Tanzania kwaajili kuazisha mradi ujulikano kama “In the Paint” ambao utahusisha ukarabati na upakaji rangi viwanja vya mpira wa vikapu vya ndani.
Akizungumza na millardayo.com & Ayo TV Mwandishi wa habari kutokea Clouds FM Kotinyo alisema… ‘NBA pamoja na MMI Tanzania wauzaji na wasambazaji wa Hennessy & Moet wameamua kuingia makubaliano ya kukuza mchezo wa Basketball na kwa kuanzia marekebisha na kuboresha uwanja wa spiders ikiwemo kuweka maeneo ya kuketi washabiki”- Kotinyo
Kwa mujibu wa meneja wa MMI Peter Kasiga alisema..“Pia kupitia mradi huu ya In the Paint utaweza kubuni na kufadhili na kurekebisha viwanja mbalimbali vya vikapu nchini kama hiki cha Spiders ambapo kutakuwa na taa na viti kulingana na idhini ya pande zote mbili kufuatilia muenendo wa uwanja wa mpira wa kikapu wa Spiders kwa muda usiopungua miaka mitatu”- Peter Kasiga
“Malengo makuu ya mradi ywa In the Paint ni pamoja na kukuza uelewa wa mpira wa kikapu na kuhamasisha ushiriki wa jamii hususani wakazi wa jiji la Dar es Salaam na utatekelezwa na pande zote mbili, kuimarisha ufahamu wa eneo la Henessy kwenye mpira wa kikapu kama washirika wa kimataifa wa shirikisho la Mpira wa Kikapu lijulikano kama NBA”– Peter Kasiga
Hapa nimekusogezea picha mbalimbali za mashabiki wa mpira wa kikapu walipofika Jumamosi iliyopita kushuhudia uwanja wa spiders ulivyoboreshwa kupitia mradi huo wa In the Paint ikiwemo kuweka maeneo ya kuketi washabiki.