Serikali imesema hakuna mfanyabiashara wa samaki anayehifadhi samaki kwa kutumia maji ya kuoshea maiti, ikiwatoa wananchi wasiwasi juu ya hofu ya kupata kansa kutokana na kutumia samaki waliohifadhiwa kwa njia hiyo.
“Jambo hili halina uhakika na kwamba watu wanahisia,” Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Hamis Ulega ameliambia Bunge mjini
Dodoma. Ulega amesema akijibu swali la nyongeza kutoka kwa Mbunge wa Viti Maalum Cecilia Pareso (CHADEMA) kuwa Makamu wa Rais Dk Philip Mpango pia ameiagiza Wizara ya Afya kufanya utafiti ili kufahamu uhalisia na kuchukua hatua za kuzuia.
“Halipo jambo la namna hiyo kwamba samaki wanavuliwa mwanza kuletwa Dodoma ama Dar es Salaam wahifadhiwe na maji ya maiti. Niwatoe wasiwasi wananchi kwamba wako salama.”
Pareso alidai kuwa “siku za karibuni tumesikia taarifa kupitia vyombo vya habari kuwa uhifadhi wa samaki kwenve baadhi va maeneo hapa chini ni wanatumia dawa za kuhifadhia maiti jambo ambalo linaleta taharuki kwa wananchi na wananchi hawajui nini cha kufanya ili wasipate hao samaki waliohifadhiwa kwa namna hiyo.”
Mbunge huyo alihoji mkakati wa serikali wa kuhakikisha samaki hawahifadhiwi hivyo na kusababisha kansa kwa watanzania.