Naibu Spika, Mussa Azzan Zungu akiwa Bungeni Dodoma leo amesema Benki na Kampuni za Simu zinakata pesa nyingi zaidi kwenye miamala inayofanywa kuliko makato ya Serikali lakini inayolaumiwa ni Serikali pekee huku akishauri Mamlaka husika kudhibiti Benki na Kampuni hizo ili zipunguze kiwango cha makato.
“Jana Serikali imetangaza kupunguza gharama za miamala lakini Wananchi wengi wanalalamikia kodi ya Serikali hawatazami mapato yanayokatwa na Makampuni ya Simu, lazima iwe regulated (idhibitiwe), unatuma pesa Benki wanachukua pesa nyingi zaidi ya Serikali kwa asilimia kubwa sana lakini Serikali imejenga madarasa na vituo vya afya ndio inalaumiwa, hili nalo mlitazame ni namna gani mtaregulate mapato ya Benki kupunguza service charge zao pamoja na kwenye miamala ya simu”