Rais Samia leo ameshiriki katika hafla ya utiaji saini Mkataba wa Usimamizi wa Shughuli za Lishe na tathmini ya sita (6) ya Mkataba wa Lishe uliofanyika Ukumbi wa Jiji la Dodoma – Mtumba, leo tarehe 30 Septemba 2022 .
“Lishe bora ni muhimu kwa Jamii, Wajawazito tunawapa lishe bora ili watoe Watoto wenye afya lakini Watoto wakizaliwa wanatakiwa pia kutunzwa na hata wakifika umri wa balehe wanapaswa kutunzwa ili wazae Watoto wenye afya ila Watoto balehe tufanye tafiti tunakosea wapi? kwanini wanakuwa na lishe mbovu? je ni masuala yaliyoingia ya mitindo? nataka niwe sijui na six packs!? nataka sijui niwe slim nisizidi kilo ngapi? nataka sijui mbavu ikae hivi?- Rais Samia
“Kwanini Watoto wetu wakifika wakati wa kuongeza Jamii wanahangaika, mara supu ya pweza…… tuna tatizo na mnalijua mnalificha, Watafiti fanyeni utafiti……. tatizo hili kwasababu halisemwi ni siri linaumiza zaidi Vijana wetu, mara sijui udongo wa Congo (vumbi la Mkongo), mara sijui kitu gani lakini tatizo kubwa lipo kwenye lishe, sasa Watafiti chunguzeni tunafanyaje Watoto wetu wawe Shababi”– Rais Samia