Shirika la Afya Duniani (WHO), limeahidi kushirikiana na serikali ya Tanzania kwa kutoa vifaa vya kutosha vya matayarisho muhimu ya kudhibiti viashiria vya tishio la ugonjwa wa Ebola.
Mtaalam wa Maabara wa Shirika la Afya (WHO) nchini, Mura Ngoi, akizungumza na waandishi wa habari Septemba 3,2022, amesema wameainisha mikoa inayohitaji mahitaji muhimu ya msaada, nguvu kazi na vitendea kazi kwa ajili ya kukinga, kudhibiti kuingia na kuenea kwa ugonjwa huo.
Ngoi amesema WHO kwa kushirikiana na serikali na kwa uzoefu wao katika nchi nyingine zenye ugonjwa huo, ikiwemo Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na Uganda, imejipanga katika kusaidia kifedha na vitendea kazi kudhibiti viashiria vya ugonjwa huo nchini.
Amesema kwa kushirikiana na Wizara ya Afya wanatoa mafunzo kwa watumishi wa afya mkoani humo katika kupambana na viashiria vya ugonjwa huo.