Katibu Mkuu Wizara ya Madini Adolf Ndunguru amewataka wafanyakazi wa wizara hiyo kuweka mazingira rafiki kwa wawekezaji ili sekta ya Madini iendelee kutoa mchango mkubwa kwenye pato la Taifa .
Ndunguru ameyasema hayo Mjini Morogoro wakati wa ufunguzi wa mkutano wa pili wa baraza la wafanyakazi wizara hiyo ambapo amesema ni wajibu wa Kila mfanyakazi kuhakikisha wanaisaidia Serikali kuvutia wawekezaji.
Ndunguru ameongeza kwa kusema kua mkutano huo ni muhimu hivyo wajumbe wanapaswa kushiriki ipasavyo kwa kutoa Michango yao ili kusaidiana sekta hiyo.
Amesema kufanya hivyo itasaidia sekta hiyo kuongeza mchango wake katika pato la taifa kutoa asimia 7.5 kwa Sasa hadi kufika asilimi 10 mwaka 2025.
Aidha amewataka wafanyakazi kuwa na ushirikiano katika utendaji kazi ili kua na mwelekeo wa pamoja katika kuimarisha sekta ya Madini.
Ndunguru amesema Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan itahakikisha kila mtanzania ananufaika kupitia sekta ya Madini kwa kukisanya mirahaba .
Amesema Madini ni Mali ya Serikali hivyo Kila mwekezaji anatakiwa kufuata kanuni na sheria za nchi huku watumishi wakisisitizwa kukusanya mirahaba kwa kufuata utaratibu uliowekwa ili Serikali iweze kupata mapato.