Makalla ametoa kauli hiyo mbele ya Rais Samia kwenye Kongamano la Kitaifa la Nishati Safi ya Kupikia leo November 01,2022 katika ukumbi wa JNICC, Dar es salaam.
“Mkoa wetu uko salama lakini nitoe taarifa kwa Wiki mbili tumekuwa kwenye changamoto Dar es salaam na Pwani ya maji, nikuhakikishie Rais Samia ulitupa Wiki mbili mradi wa maji wa Kigamboni uwe umefanya kazi ili kupunguza makali ya mgao wa maji Dar es salaam, ninayo furaha kuripoti kwako kwamba usiku wa leo tunaingiza maji kutoka Kigamboni katika visima 12 ambapo wewe (Rais Samia) umetoa Tsh. Bilioni 23, lita Milion 70 zitaingia Mjini ili kupunguza ukali wa mgao wa maji”– RC Makalla
“Nimefika kwenye vyanzo vyote vya maji Ruvu chini na Ruvu juu, tatizo la mgao ni ukame ambapo tunategemea mvua lakini Mamlaka ya Hali ya Hewa ilishatabiri kutakuwa na ukame chanzo cha ukosefu wa maji ni kudra za Mungu sio Ilani ya CCM maana Ilani haiwezi kutaja italeta mvua”- RC Makalla