Mbunge wa Jimbo la Ushetu Mheshimiwa Emmanuel Peter Cherehani ameiomba serikali kutilia mkazo kilimo cha umwagiliaji kupitia mradi wa maji wa Ziwa Victoria unaoanzia jijini Mwanza mpaka Tabora mjini, mradi ambao utawasaidia wakulima kunufaika na kilimo cha umwagiliaji.
Mheshimiwa Cherehani ameyasema leo bungeni jijini Dodoma katika mkutano wa 9 kikao cha saba ambapo ameshauri serikali kuchimba mabwawa makubwa yatayotumika na wakulima katika shughuli za kilimo na kuachana na kilimo cha kutegemea mvua.