Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wamemchangia Tsh 5,023,000 Kijana Majaliwa Joseph, aliyesaidia kuokolewa kwa Watu 24 katika ajali ya ndege ya Precision Air iliyotokea katika Ziwa Victoria November 6 mwaka huu.
Hoja hiyo ilianza kwa Mbunge wa Nzega vijijini, Hamis Kigwangalla ambaye alisimama na kuomba kuomba Muongozo kwa Spika, ili aelekeze Wabunge wachange 50,000 kila mmoja kutoka kwenye posho zao za siku na kumpatia Majaliwa Jackson kama ishara na alama ya kutambua mchango wake mkubwa.
Spika, Dr Tulia Ackson akitoa muongozo amesema kwa kutumia kanuni Kigwangalla alipaswa kutoa hoja, wabunge waunge mkono lakini hakufanya hivyo hivyo Spika alitoa muongozo Wahudumu kupita kwenye viti vya Wabunge kukusanya michango na baadaye akatangaza kupatikana kwa Tsh 5,023,000.