Rais Samia akiwa Arusha leo amefungua Mkutano wa 27 wa Jumuiya ya Wanasheria Afrika Mashariki ambapo amesema Tanzania imeamua kuzingatia misingi ya haki na inajitahidi kujenga Taifa la haki, demokrasia, usawa na mafanikio ikiwa ni pamoja na kukubali kukosoana na anayekosolewa akubali kujikosoa.
“Mafanikio yoyote ya kiuchumi yanayotokana na mbinu zinazokiuka misingi ya haki hayawezi kuwa endelevu hata siku moja, kutenda haki na kuheshimu utawala bora ni misingi ambayo Serikali yoyote inayotokana na Watu haina budi kuifuata bila shinikizo lolote kutoka nje”
“Na Serikali ya Watu maana yake imepigiwa kura na Watu, imekaa kwa utashi wa Watu, haina budi kufuata misingi ya haki, isipofuata misingi hiyo Serikali sio ya Watu, Tanzania tumeamua kuizingatia misingi hiyo na tutajitahidi kuijenga Tanzania yenye haki, demokrasia, usawa na mafanikio”
“Tutaendelea na jitihada za kusikiliza kila Mtu, wapi kuna gape tukubali kukosoana, na anayekosolewa akubali kujikosoa, then turekebishe tuende na mambo yetu, na haya si matamanio ya Serikali ya awamu moja ama nyingine, ni matakwa na misingi ya Katiba yetu”