Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) Masanja Kadogosa ametoa ufafanuzi juu ya kauli na mijadala iliyopo mitandaoni kuhusu Mabehewa mapya ya Reli ya Kisasa (SGR) ni ya mtumba na yamenunuliwa kwa gharama kubwa.
“Yale Mabehewa sio ya mtumba wala used ni Mabehewa mapya, sasa anayezungumza mnaweza kumuuliza vyanzo vyake ni wapi anapata, ni Mabehewa yaliyokuwa yakitengezwa kwa miaka miwili, katika manunuzi kuna sheria ambapo lazima kabla hamjasema huyu hapa tunaenda nae lazima kuwe na ulinganifu wa bei, sasa Mtu anapoibuka tu na kuanza kusema mabehew yana kiasi fulani ni jambo la ajabu kidogo ila mtamuuliza yeye”
“Kuhusu bei ya Mabehewa yapo 59 na sio 14 yamekuja kwa awamu ya kwanza, mwaka kesho Mei tutapata mengine 45 jumla yatafanya kuwa 49 na bei aliyoitoa bei ni Dola Milioni 55.6 ndio bei ya Mabehewa”