Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini Mrisho Gambo amesema amefanyiwa uvamizi mara mbili nyumbani kwake Jijini Arusha na Watu ambao ni Viongozi wa Serikali na anawafahamu.
Gambo ametoa tuhuma hizo leo akiwa kwenye mkutano wa hadhara katika eneo la Soko Kuu Arusha alikoongea yafuatayo “Wamejaribu sababu zote wameshindwa Mimi mwenyewe nyumbani kwangu binafsi wameshanivamia mara mbili na walionivamia nawafahamu ni Viongozi wa Serikali”