Takribani vijana 300 kutoka katika Vyuo Vikuu na Vyakati nchini wanatarajia kushiriki kwa pamoja katika Mkesha wa Vijana Karismatiki wa Vyuo Vikuu jimbo Kuu la Dar es Salaam kwa ajili ya kuliombea taifa.
Mbali na hilo pia ibada hiyo itaendana na maombi ya vijana kujiepusha na mmomonyoko wa maadili.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Katibu Maandalizi ya Usiku wa Sifa, Ronaldo Chota amesema….“Tunaamini vijana watakaoudhuria mkesha huu pamoja na mmomonyoko wa maadili ambao tunauona ikiwemo kuiga tamaduni kwanza uwepo wa Mungu na ibada ya Misa watapata mafundisho ya hofu ya Mungu itakayowasaidia kuacha tabia za kutompendeza Mungu,”
Kwa Upande wake, Padri wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Vitalis Kassembo amesema…”wameandaa mkesha mkubwa ambao utafanyika usiku wa Ijumaa kuamkia Jumamosi na lengo ni Uinjilishaji wenye sura mbalimbali anbapo hii ni kwa njia ya mkesha, tunakesha kusubiri kile ambacho Mungu ametuandalia kwani tunaamini kuna maisha baada ya kuondoka hapa duniani, kwahiyo tunakesha,”.
Naye Ludovick Kawishe ambaye ni Paroko wa Parokia ya Mburahati amesema, “Ni nafasi ya pekee kuwainjilisha vijana hivyo tunamshukuru Baba kwa kutupa hii nafasi, hii ni fursa ya pekee sana, tunashukuru vijana wa Vyuo ambao wamepata haya maono ya kuwawezesha kufanya huo mkesha,”