Utalii wa Tanzania umegeuka kivutio nchini Qatar kutokana na wageni wa mataifa mbalimbali kufika katika banda la Tanzania lilipo kwenye Maonesho Maalumu ya Kutangaza Utalii na Uwekezaji katika nchini hiyo.
Akizungumza na Ayo Tv na Millardayo.com kutokea nchini Qatar ambapo michuano ya Kombe la Dunia inaendelea, Afisa Utalii Mkuu, Elirehema Maturo amesema idadi ya kubwa ya wageni imeahidi kutembelea vivutio vya utalii nchini Tanzania.
“Watalii wengi wanapofika kwenye banda letu wamekuwa wanauliza maswali mengi na wamevutiwa zaidi na vivutio na vifurushi vya utalii wa Picha na Uwindaji wa Kitalii unaofanyika katika mapori ya akiba na yale tengefu,”.
“Pia wageni wengi kutoka hapa Qatar na nchi za Mashariki ya Kati wamevutiwa zaidi na vifurushi vya uwindaji wa kitalii vyenye Wanyamapori hadimu wasiopatikana katika nchi nyingine duniani,”amesema.
Maonesho hayo yalianza Novemba 18 na yatamalizika Disemba 18,2022 huku ikielezwa kwamba huo ni mkakati wa Rais wa Tanzania Dr.Samia Sukuhu Hassan katika kukuza sekta ya utalii nchini.