Mahakama ya Wilaya ya Kigamboni jijini Dares Salaam imemhukumu kifungo cha miaka 30 jela mshatakiwa Ally Yusuph Issa maarufu kama Mpeche, kwa kosa la kusafirisha dawa za kulevya aina ya heroin.
Hukumu hiyo imetolewa siku ya ljumaa tarehe 30 Disemba 2022 na Hakimu Mgaya baada ya mtuhumiwa kukiri kosa la kusafirisha dawa hizo kinyume cha sheria.
Ally alikamatwa tarehe 9 Disemba, 2022 katika eneo la Kibugumo kwa mbuzi wilaya ya Kigamboni jijini Dar es Salaam akiwa na wenzake wawili ambao ni Abdulrahman Ally Sinauwanja Mariam Yahya Fundi wakiwa na gramu 75.62 za dawa za kulevya aina ya heroin na kufunguliwa kesi ya jinai namba 89 ya mwaka 2022.
Hata hivyo, washtakiwa wengine wawili walikana shtaka hilo, hivyo kesi dhidi yao inatarajwa kutajwa mahakamani hapo tarehe 4 Januari 2023.