Waziri wa Afya Ummy Mwalimu ametoa taarifa kuhusu video inayosambaa mtandaoni ikiwaonesha Watumishi wa Afya wakivutana kwa maneno huku mmoja akionekana kupinga kitendo cha vifaa tiba vilivyopita muda wake kutumika.
Ummy amesema Timu ya Usimamizi Afya ya Mkoa (RHMT) wa Tabora na ya Halmashauri (CHMT) ya Wilaya ya Uyui wanafuatilia suala hili na Serikali itatoa taarifa kwa umma juu ya hatua zilizochukuliwa “Tunawashukuru wote walioibua suala hili”
View this post on Instagram