Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amemteua Emmanuel Mpawe Tutuba, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango kuwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) akichukua nafasi ya Prof. Florens Luoga ambaye amemaliza kipindi chake.
Rais amemteua pia Dkt. Natu El- Maamry Mwamba kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Mwamba alikuwa Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dares Salaam na Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Uendeshaji
wa Kiwanja cha Ndege cha Kilimanjaro (KADCO).
Dkt. Mwamba anachukua nafasi ya Emmanuel M. Tutuba ambaye ameteuliwa kuwa Gavana wa Benki Kuu.