Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana UVCCM, Ali Mohamed Kawaida, amemuomba Rais na Amiri Jeshi Mkuu, Dkt Samia Suluhu Hassan Vijana wafupi nao wapate nafasi jeshini tofauti na ilivyo sasa, ambapo amesema Vijana warefu wanapewa zaidi kipaumbele kuliko wafupi katika Jeshi la Polisi.
Amesema hayo leo January 10, 2023 alipokuwa katika kilele cha matembezi ya UVCCM ya kuadhimisha miaka 59 ya mapinduzi matukufu ya Zanzibar.
“Vijana wa Kitanzania wamenituma nije na ombi hili kwako Rais, ombi la Vijana wa Kitanzania kwa Jeshi la Polisi, hatujui kama ni kanuni, utaratibu ama ni sheria yao ya kuwakataa Vijana wenye asili ya ufupi na kuchukua tu Vijana wenye asili ya urefu, huku ni kutukataa wafupi, wakisahau kwamba jukumu la ulinzi na usalama wa Taifa ni la Vijana wote tukiwemo sisi wafupi”- Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana UVCCM Ali Mohamed Kawaida.