Serikali imesema kuwa bei za vyakula nchini zitashuka kuanzia mwezi Machi hadi Aprili, mwaka huu kutokana na wingi wa vyakula hayo yamebainishwa jijinj Dodoma leo Januari 10, 2023 na Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe wakati akizungumza na Wahariri wa Vyombo vya Habari kuhusu mikakati ya wizara hiyo ya sasa na ya baadae.
“Kama waziri naweza kusema kwamba bei ya chakula itashuka kuanzia mwezi Machi hadi Aprili, mwaka huu kwani vyakula vitakuwa vingi.
“Hivyo, nikiri kwamba ni kweli tuna changamoto ya bei lakini ni kipindi cha mpito tu na baadae bei itashuka. Siyo kwamba wizara ya kilimo hatuelewi upandaji wa bei ya vyakula,” amesema Waziri Bashe. Aidha, Bashe ametaja gharama za usafirishaji kuwa ni moja ya sabahu inayochochea kupaa kwa bei ya vyakula nchini nakwamba wanaimani kuwa zitashuka kufikia kipindi hicho.