Chama Cha Wamiliki wa Malori Tanzania-TATOA kimesema kitawakutanisha wadau wa sekta ya uchukuzi ili kujadiliana masuala mbalimbali ya sekta ya usafirishaji.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa TATOA, Elias Lukumay amesema huo ni Mkutano Mkuu wa 7 wa Mwaka utakaofanyika Januari 21, 2023.
“Tutajadili masuala mbalimbali yanayohusiana na sekta ya usafirshaji, hii inajumuisha changamoto zote zinazoikabili sekta ya usafirishaji,Mkutano huo utajumuisha wadhamini ambao watakuwa wakiwasilisha,kuonyesha bidhaa na huduma zao ambazo zinaongeza utendaji kazi katika sekta ya usafirishaji”– Elias Lukumay
Kwa upande wake, Meneja Masomo na Mawasiliano wa GF, Smart Deus amesema mkutano huo unatarajiwa kutoa fursa hasa katika sekta ya uwekezaji.
“Mwaka huu kuelekea mwisho wa Januari tunatarajia kuzindua gari ambayo tumei- assemble hapa Tanzania lakini sisi ni wausaji wakubwa wa magari, hivyo wanachana watakaoshiriki mkutano wa TATOA wanatakiwa kufikia GF,” amesema Smart.