Imeelezwa kuwa Takriban wawekezaji 3800 wamejiandikisha kuwekeza katika mfuko wa FAIDA FUND jambo ambalo limefanikisha makusanyo ya Shilingi Bill 13.5 kwa kipindi kifupi.
Hayo yameelezwa jijini Dar es salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa Watumishi Housing Investmet Dkt. Fredy Msemwa ambapo amesema kiwango cha uwekezaji katika mfuko huo kimeendelea kukua siku hadi siku na hivyo kuongeza mafanikio ya mfuko huo.
Amesema kuwa mpaka wanafunga mauzo ya mwanzo tarehe 31 Disemba mwaka 2022 wamefanikiwa kukusanya kiwango kikubwa na hivyo kuvuka malengo yaliyokuwa yamewekwa
Dkt. Msemwa amesema kuwa mafanikio hayo yanatokana na watu wengi wamekuwa wakitumia teknolojia rahisi na matumizi ya simu na mitandao ya kompyuta imesaidia kuufikia mfuko huo kwa wepesi na hivyo kufanikisha makusanyo hayo.
‘Watu wengi wameweza kufikia mfuko wa FAIDA FUND na kufanya uwekezaji ambao tumeweza kukusanya kiasi cha Tsh Bill 12.95 ambacho kilikuaanywa tarehe 31.12.2022 na hivi sasa kiasi hicho kimeongezeka mpaka kufika jana kwenye mwezi huu tumekusanya Shilingi Bill 13.5’amesema Dkt. Fredy Msemwa
Aidha Dkt. Msemwa amesema kiasi cha fedha ambacho kimewekezwa kimeendelea kukua siku hadi siku ambapo pia thamani ya kipande awali ilikuwa 100 na sasa imeongezeka kwa shilingi 100.54 mpaka kufika jana.
Mkurugenzi huyo amesema mafanikio hayo yamewezekana kutokana na matumizi ya mfumo rahisi wa malipo serikali ambao umewaletea faida kubwa ikiwemo ya utambuzi wa miamala kufanyika kwa kasi kubwa.
Dkt. Msemwa ameeleza faida nyingine kuwa yanafanya fedha zinazowekezwa kuwa salama ambapo tayari fedha hizo zimeingizwa katika uwekezaji wa dhamana za serikali za muda mrefu miaka 2022/2025
Hata hivyo wawekezaji pia wamepata faida katika Mfuko huo kutokana na gharama zake kuwa ndogo kwani wanalipa kidogo kwa ajili ya mtandao na zinazobaki zinaingizwa serikalini.