Watu 16 akiwemo Waziri wa Mambo ya Ndani wa Ukraine na maafisa wengine wakuu wa wizara wamepoteza maisha katika ajali ya helikopta iliyotokea nje ya Mji Mkuu wa Kyiv leo hii.
Taarifa ya Mkuu wa Polisi Ukraine, Ihor Klymenko amesema kati ya watu hao waliopoteza maisha wawili ni watoto, tisa kati ya waliouawa walikuwa ndani ya helikopta ya huduma za dharura.
Amesema watu 22 wamejeruhiwa katika ajali hiyo wakiwemo watoto 10 huku taarifa zikieleza kuwa helikopta hiyo imeanguka karibu na jengo la shule ya watoto eneo la Brovary huko Kyiv.
Kwa mujibu wa Klymenko waliopoteza maisha ni Waziri wa Mambo ya Ndani, Denys Monastyrskyi, naibu wake Yevhen Yenin na Katibu wa Jimbo la Wizara ya Mambo ya Ndani, Yurii Lubkovych na wengine.
Aidha, hakuna taarifa za moja kwa moja zinazohusisha chanzo cha ajali hiyo,imeripotiwa kuwa uchunguzi utaanza mara moja kubaini chanzo cha ajali hiyo.
MWANZO MWISHO KIFO KILIVYOCHUKUA STAA WA KUCHEZA NA PIKIPIKI, BABA ASIMULIA HISTORIA