Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky amesema hakuna ushahidi wa moja kwa moja kwa Taifa la Urusi kuhusika na ajali ya helikopta iliyotokea jana katika jiji la Kyiv na kuuwa watu 18 akiwemo Waziri wa Mambo ya Ndani na naibu wake.
Akizungumza jana katika Kongamano la Kiuchumi la Dunia huko Davos nchini Uswis, Zelensky alisema licha ya kwamba hakuna anayehusika na tukio hilo ila kitendo kilichofanywa kwenye taifa lake ni matokeo ya vita inayoendelea nchini kwake.
“Wakati ambao ulimwengu huru hutumia kufikiria unatumiwa na serikali ya kigaidi kuua,” alielezea. Matamshi hayo yametafsiriwa kama ombi kwa Ujerumani kuharakisha kuwasilisha mizinga yake ya Leopard inayotamaniwa na Ukraine.
Imeripotiwa kuwa Ujerumani haiko tayari kupeleka magari ya silaha isipokuwa Marekani itajitolea kutoa mizinga yake ya kivita ya Abrams. Wiki iliyopita Uingereza iliahidi kutuma mizinga yake kadhaa huko Kyiv.
Mkuu wa muungano wa kijeshi wa Nato alisema huko Davos jana kwamba Ukraine inaweza kupokea msaada zaidi, usaidizi wa hali ya juu zaidi, silaha nzito zaidi na silaha za kisasa zaidi.el