Staa wa soka wa zamani wa Barcelona na Timu ya Taifa ya Brazil Deni Alves (39) amekamatwa na anafanyiwa uchunguzi dhidi ya tuhuma zake za kumfanyia unyanyasaji wa kijinsia mwanamke mmoja nchini Hispania.
Alves (39) amewekwa ndani bila dhamana yoyote kufuatia tukio lake hilo alilodaiwa kufanya katika club ya usiku ya Sutton jijini Barcelona.
Baada ya jaji kuagizwa Alves awekwe ndani bila dhamana Club yake ya Pumas ya nchini Mexico imetangaza kuvunja mkataba na mchezaji huyo, Alves alikuwa Barcelona wakati wa mapumziko ya sikukuu na mambo ya kifamilia.