Simba SC imemtangaza Imani Kajula kuwa Afisa Mtendaji Mkuu wao mpya (CEO) ambaye anachukua nafasi ya Barbara Gonzalez aliyemaliza muda wake.
Imani Kajula ambaye alikuwa CEO wa EAG Group ambayo ni Kampuni ya Masoko na Mawasiliano ana uzoezi wa kufanya kazi katika masuala ya masoko na biashara kwa zaidi ya miaka 20.
Imani hadi anatangazwa kujiunga na Simba SC alikuwa CEO wa EAG Group kuanzia 2013, kabla ya hapo alikuwa Mkuu wa Masoko na Mawasiliano NMB (2006-2013), Mkurugenzi wa Masoko na Maendeleo ya Biashara wa Tanzania Postal Bank (2003-2006) na alikuwa Meneja Masoko CRDB Bank (1999-2003).