Mwili wa Mtanzania Nemes Tarimo ambaye alifariki October 24,2022 akiwa vitani nchini Ukraine baada ya kujiunga na Jeshi binafsi la Urusi la Wagner Group umefikishwa nyumbani kwa Familia Mbezi Dar es salaam baada ya kupokewa katika Uwanja wa Ndege wa J.K Nyerere Dar es salaam leo January 27,2023 ambapo utaagwa na kusafirishwa leo hadi Mbeya kwa maziko.
Kwa mujibu wa taarifa ya Serikali ya Tanzania iliyotolewa na Waziri wa Mambo ya Nje ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki mapema Wiki hii, Nemes alifariki akiwa vitani nchini Ukraine baada ya kujiunga na Jeshi binafsi la Urusi la Wagner Group akiwa anatumikia sehemu ya kifungo chake cha miaka saba alichofungwa kwa makosa ya kihalifu.
Waziri Tax alinukuliwa akisema “Tarimo akiwa gerezani alipewa nafasi ya kujiunga na kikundi cha kijeshi cha Wagner kwa ahadi ya kulipwa fedha lakini kwa ahadi ya kuachiwa huru mara baada ya vita na umauti ulimkuta October 24,2022 na Wizara ikawasiliana na Serikali ya Urusi ili kukabidhiwa mwili”