Baraza la Ulamaa katika kikao chake cha dharura kilichojadili nambo mbalimbali kilichofanyika January 27, 2023 kimetengua uamuzi wenu wa kuivunja Ndoa ya ndugu Juma Mwaka na Bi Queen Oscar Masanja kwa kuhukumiwa katika Mhimili usiohusika kinyume na mhimili wa Mahakama ya Kadhia.
Kesi hiyo Shauri No 041/2022 linatakiwa kuendelea katika mhimili wake wa awali mhimli wa Mahakama ya Kadhi wenye taratibu na misingi ya kisheria tangu zama za mtume Muhammad SAW na pale mlalamikaji au mlalamikiwa asiporidhika na uamuzi atatakiwa akate rufaa katika ngazi ya juu ya Mahakama ya kadhi Kwa kadhi Mkuu na kamwe si vinginevyo.
Baraza la Ulamaa linakutaka uacha mara moja nia yako ya kuligeuza Baraza la Mashekhe Mkoa na kulifanya kuwa ndio Mahakama ya Kadhi,
Kwa barua hii Baraza la Ulamaa linakuagiza kuyaacha maswala yote yaliovuka ngazi ya usuluhishi na kuhamia katika Mahakama ya kdhi, Uyaache yaendeshwe katika Mhimili huo huo bila kuyaingiali hadi Mwisho.