Mkuu wa Mkoa wa Kagera Albert Chalamila amewaapisha wakuu wapya wa Wilaya tatu za Mkoani humo,na kupitia hafla hiyo ametoa maagizo kwa Kamanda wa Polisi na Mkuu Mpya wa Wilaya ya Bukoba Erasto Sima kuanza kuchukua hatua na kufanyia kazi maelekezo yake ikiwemo agizo la kuwakamata baadhi ya viongozi Wilayani humo
“Kuna baadhi ya wazazi wanaoozesha watoto na hawataki watoto hao kusoma,nakupa jukumu hapahapa sasa hivi,kijiji cha Karonge Kata ya Ibwera kuna Binti ameozeshwa na kufunga ndoa na wamelipa mahari na Diwani anafahamu na anafurukuta kujaribu kuweza kuwatetea wale wazazi waliowatorosha na kuwaozesha,sasa RPC mtafute Diwani wa Ibwera na ushahidi wote ninao hapa katafuteni hata wazazi wa huyu binti Kamata watu hawa wakalisheni kunakostahili watoe ushirikiano na huyu ni binti aliyekuwa anasoma shule ya Msingi Rubaga”- RC Chalamila