Maafisa katika mji wa kibiashara wa Afrika Kusini , Johannesburg,wameanza uchunguzi baada ya mkazi kubaini maji yenye rangi ya bluu yakitiririka kwenye bombo lake.
Mkazi huyo alikuwa amesambaza picha Jumatatu pamoja na video za uzoefu wake huo wa kutisha kwenye mitandao ya kijamii.
Msemaji wa kampuni ya usambazaji maji , Johannesburg Water, ilisema kuwa inashuku maji hayo yalikuwa yamechafuliwa na shaba iliyopo katika jengo hilo, lakini sampuli zimechukuliwa kwa ajili ya kufanyiwa kipimo, kulingana na taarifa za nchini humo.
Matokeo yanatarajiwa kutolewa katika kipindi cha saa 24 baada ya sampuli hizo kufanyiwa uchunguzi, Puleng Mopeli alinukuliwa akisema.
Mkazi aliyeathirwa ameuambia mtandao wa habar wa IOL news kwamba maji ya bluu hatimaye yaliacha kutoka.
There’s some coming out now again and they’re still blue, just lighter in colour … angisazi.@CityofJoburgZA @JHBWater can anyone at least let us know what this blue colour is in the water? Is it normal or safe? We are still water shedding in our area btw 🙃 pic.twitter.com/UrcTELA8T5
— Ntombi M (@_ntombim_) January 30, 2023