Katika kukabiliana na magonjwa ya milipuko, Jeshi la Polisi wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro wameshirikiana na Wananchi katika shughuli za kijamii ikiwemo kufanya Usafi.
Akizungumza Katika zoezi hilo Kamanda wa Wilaya ya Same (OCD) SSP Phinias Majula alisema wao kama jJshi la polisi wameona ni vyema kushirikiana na Jamii kwenye zoezi la kusafisha mazingira kuepuka milipuko ya magonjwa kama kipindupindu lakini pia kuona sehemu zinakuwa safi na salama.
Pia aliendelea kutoa wito kwa Wananchi wote nchi nzima kutunza mazingira safi na salama na kupendelea kufanya Usafi kwenye eneo linalo kuzunguka hili kuepukana na magonjwa ya Milipuko.
Kamanda Majula aliwaomba Wananchi kuendelea kushirikiana na jeshi la polisi kwa kutoa taharifa za huwalifu na wahalifu katika wilaya hiyo. Kwani ni jukumu lao kuwalinda wananchi na Mali zao.
Afisa Mtendaji Mkuu mamlaka ya mji mdogo wilaya ya Same amesema kwa niaba ya Mkurungezi Mkuu wilaya ya Same Anastazia Tutuba ametoa shukrani za dhati kwa jeshi la polisi kushirikiana na wananchi kwenye shughuli za kijamii.
Pia ameliomba Jeshi la Polisi kuendelea na utamaduni wa kushirikiana na Wananchi lengo ni kujenga husiano mzuri baina ya Jeshi na Wananchi.