Zaidi ya watu 60809 wamepata Elimu ya Sheria mkoani Morogoro Kwa kipindi cha wiki Moja kuanzia januari 26 hadi February 1 mwaka huu
Akizungunza wakati wa kilele Cha wiki ya Sheria Jaji Mfawidhi wa mahakama kuu ya Tanzania kanda ya Morogoro Mheshimiwa jaji Paul Ngwembe amesema watu hao wamepata Elimu hiyo Kwa njia mbalimbali ikiwemo ana kwa ana,vipeperushi na Vyombo vya Habari.
Mheshimiwa Jaji Ngwembe anasema idadi ya watu waliopata Elimu ya sheria imeongezeka kutoka 33567 mwaka 2021/ 2022 hadi kufikia watu 60809 mwaka 2022/ 2023.
Anasema lengo la Kutoa Elimu hiyo ni Kuhakikisha wananchi wanapata ufahamu kuhusu masuala ya sheria ambapo wananchi wengi wamekua wakifungwa Kwa kutokujua sheria Jambo ambalo halina utetezi kwenye utoaji haki huku jina ya usulihishi ikisisitiswa zaidi Kwa Jamii.
Anasema Elimu hiyo imesaidia kwani mwaka 2021 makosa ya ubakaji yalikua 196,Ulawiti 32, mauaji 95 ,madawa ya kulevya 188 na nyara za serikali 53 jumla yakiwa malalamiko 567 ambapo mwaka 2022 yamepungua na kufikia jumla ya malalamiko 464 Kwa ufafanuzi wa ubakaji 156,Ulawiti 24,mauaji 66 ,madawa ya kulevya 141 na nyara za serikali 77.
Kwa upande wake mkuu wa Mkoa Morogoro amewataka mahakimu na majaji kutumia busara pindi wanapotoa hukumu kwani kuna baadhi ya wananchi wamekua na malalamiko ya uongo na kuleta sintofahamu katika vyombo vya kutokea Haki.
Aidha RC Mwassa amewataka wananchi kufuata Sheria wakati wakihitaji umilikishwaji wa ardhi ili kupunguza Migogoro ya ardhi kwenye vijiji ambayo imekua changamoto hasa maeneo mengi ya Mkoa huo.