Shirikisho la Kimataifa la Historia na Takwimu za mpira wa miguu duniani (IFFHS) limeitangaza Ligi Kuu ya Tanzania bara (NPL) kuwa Ligi ya tano (5) kwa ubora Afrika na 39 duniani kwa mwaka 2022.
Taarifa hiyo iliyotolewa na tovuti ya IFFHS January 19 2023 imeonesha Ligi ya Tanzania imepanda kidunia kutoka nafasi ya 62 kwa mwaka 2021 hadi 39 kwa mwaka 2022.
Ligi namba 1 kwa Afrika kwa mujibu ya IFFHS ni Misri, Algeria, Morocco, Sudan wakati kidunia Brazil imeendelea kuwa namba 1 na England imeendelea kuwa namba 2.