Tafiti zinaonesha kitendo cha kuwaruhusu Watoto wenye umri mdogo kutumia computer na kutazama TV kwa muda mrefu kunaweza kupunguza mafanikio yao ya kitaaluma na uwezo wa kihisia ifikapo miaka ya baadaye, kulingana na utafiti mpya.
Watafiti wamegundua kuwa kuongezeka kwa muda ambao unatumika na Watoto wenye umri mdogo kwenye vifaa kama simu, vishkwambi na computer kunahusishwa na utendaji duni pindi Mtoto anapofikisha umri wa miaka 9, kulingana na utafiti uliochapishwa mapema wiki hii katika jarida la JAMA Pediatrics kutokea nchini Marekani.
Uwezo wa utendaji kazi wa Mtoto ni michakato ya kiakili ambayo humuwezesha kupanga, kuzingatia uangalifu, kukumbuka maagizo yaliyotolewa na kushughulikia kazi nyingi kwa mafanikio kwa mujibu wa Kituo cha Chuo Kikuu cha Harvard.
Dk. Erika Chiappini, Profesa Msaidizi wa Sayansi ya Akili Chuo Kikuu cha Johns Hopkins Jijini Baltimore nchini Marekani anasema utendaji kazi ni muhimu kwa ukuaji wa Mtoto kwa kiwango cha juu kama vile kwenye udhibiti wa kihisia, uwezo wake wa kujifunza, mafanikio ya kitaaluma atakapo kuwa masomoni pamoja na afya ya akili.
Matokeo hayo yanaunga mkono mapendekezo kutokea Chuo cha Marekani cha Madaktari wa Watoto, ambacho hupinga ongezeko la muda wa kutumia skrini kabla ya umri wa miezi 18, isipokuwa kwenye video calls.