Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) kupitia bia yake ya PILSNER imetenga Tsh. milioni 36 kwa ajili ya kuwazawadia Watanzania 12 wataoshinda katika kampeni yake ya “Kapu la Wana” ambayo ina zawadi mbalimbali kama gari, bodaboda, TV na simu za mkononi ambapo Meneja wa Bia hiyo Wankyo Marando amesema siku zote bia hiyo ipo kwa ajili ya kusherehekea mafanikio ya walaji na kuwatunza kwa umaridadi wao kwenye kutimiza ndoto na kuchapa kazi.
“Kampeni hii itadumu kwa miezi 8, Pilsner Lager ni bia ya Vijana ambao hawakati tamaa na wenye kiu ya kutimiza mafanikio makubwa, tunawawezesha Vijana kwa kuwapatia vitendea kazi ili wasonge mbele hivyo tunawahamasisha walaji wote wa PILSNER LAGER kuitumia kampeni hii ili kusogeza juhudi zao mbele” Wankyo Marando.
“Ukinunua bia ya Pilsner Lager utapata kadi ya kukwangua ili kujipata zawadi kila ununuapo bia kama zawadi ni bidhaa kama fulana, kofia utazawadiwa papohapo na kama zawadi uliyoikwangua ni namba maalum, itume kupitia ujumbe mfupi wa maneno (SMS) kwa namba 15320 mfano: Andika Kapu 4321 Iringa (acha nafasi), Mshiriki lazima awe na miaka 18 na kuendelea”
Miongoni mwa waliokuwepo kwenye Mkutano huu na Waandishi wa Habari ni Afisa Mkaguzi Salimu kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha pamoja na Mshindi wa “kapu la wana” wa mwaka 2022 Vicent Kimario ambaye amesema anaishukuru Kampuni ya Serengeti kwa kuweza kutoa fursa mbalimbali kwa Vijana hivyo wachangamkie fursa ili kubadilisha maisha.