BAADA kimya cha muda mrefu, tamasha la Pasaka sasa litafanyika Aprili 9,2023 jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Msama Promotion ambao ni waandaaji wa tamasha hilo, Alex Msama amesema tamasha hilo litakua la aina tofauti kwa kuwa waimbaji wote wataimba live.
“Kuna wasanii wengi wakubwa wa mziki wa injili kutoka nje watakua, kuna ambao hawajawahi kufika Tanzania, ndio itakua mara ya kwanza. “Amesema Msama
Amesema, kwa sasa wameanza kuweka mambo sawa kuhakikisha tamasha hilo pendwa linafanyika ubora na kishindo kikubwa.
“Wapenzi na washabiki wa nyimbo za injili wakae mkao wa kuzikosha nafsi zao huku wakimtukuza Mungu kwa nyimbo za Injili. ”Tulikuwa kimya kwa muda mrefu kwa sababu mbalimbali,lakini kwa sasa tumeamua kurudi upya na tamasha letu pendwa la Pasaka.”Amesema Msama
Amesema tamasha hilo ambalo mara ya mwisho lilifanyika mwaka 2015 mbali na Dar es Salaam pia litafanyika katika mikoa ya Mwanza, Arusha na Dodoma.