Mwimbaji Staa wa Bongofleva Omari Mwanga maarufu Marioo ameishukuru GSM Tanzania kupitia Kampuni yake ya GSM HOME kwa kuubadilisha muonekano na kuupamba mjengo anaoishi Mikocheni Dar es salaam aliohamia December 2022.
GSM Home yenye maduka yake ya vitu vya nyumbani kwenye kona mbalimbali za Dar es salaam ikiwemo Masaki na Mikocheni, wameubadilisha muonekano wa mjengo huu ikiwa ni zaidi ya mwezi mmoja umepita toka alipou-post kwenye mitandao yake ya kijamii.
December 2022 akihojiwa kwenye Interview na XXL ya CloudsFM kuhusu Mjengo wake, Marioo alisema yafuatayo ———> “Ni kweli mziki unalipa kwa sababu hata kama ni kupanga ile nyumba sio chini ya dola elfu mbili kwa mwezi ambayo ni zaidi ya milioni 4, unaweza kuona jinsi tunavyopata mafaniko mara nyingi tunakesha mastudio so inabidi tuwe na mazingira mazuri ya kuegesha, kukaa kwenye balcony kula upepo”
View this post on Instagram