Watu zaidi ya 20 wamenusurika kufa baada ya kutokea kwa ajali ya gari ya abiria aina ya daladala inayofanya safari zake kutokea Olorieni na coaster kugongana uso kwa uso katika eneo la kibo palace Uzunguni Arusha.
Kwa mujibu wa Julius Daniel ambaye ji abiria aliyekuwa amekaa mbele ya gari hiyo ya abiria amesema gari hiyo ilikuwa ikiendeshwa kwa mwendo kasi huku ikitaka kuipita gari nyingine kwa mbele nakusababisha ajali hiyo.
“Tulikuwa tupo kwenye spidi gari ya mbele yetu ikashika brake gafla,hakuweza kusimama gafla aka overtake akakutana na coaster wakagongana uso kwa uso”