Baada ya kuibuka maswali mengi yakitaka kufahamu hali ya Mtu anaeonekana anagongwa na basi la abiria la Mwendokasi lililogonga na gari dogo maeneo ya Kisutu, AyoTV imeamkia Taasisi ya Mifupa MOI ambapo ndipo amelazwa huyo.
Meneja wa Kitengo Uhusiano MOI Patrick Mvungi anasema mtu huyo wamempa jina la ‘UNKNOWN’ maana mpaka sasa hawana taarifa zake rasmi na amelazwa ICU.
Kwa mujibu wa Mvungi mpaka sasa ‘UNKNOWN’ hawezi kuongea ila anafungua macho na baadhi ya viungo “ Kavunjika mguu, mkono na ameumia kivhwani”