Kiwanda kikubwa cha smart card ambacho kimejengwa mwaka jana Mkoani Tanga kinatajwa kuwa kitasaidia Serikali kuondokana na changamoto ya kuagiza card kama za NIDA, leseni na kadi za ATM nje ya nchi.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga Omary Mgumba ametembelea kiwanda hicho cha Rushabh Investment cha kutengeneza smart card ambapo amesema kiwanda hicho ni cha kwanza hapa nchini na cha pili Africa kinachotengeneza card ambapo kipo kwenye majaribio ili kuanza rasmi uzalishaji ambao utasaidia Serikali kutoagiza kadi nje.
“Kama tulivyoona pale wapo kwenye majaribio ya kutengeneza card hizi kama vile vitambulisho vya NIDA, kadi za ATM, leseni n.k, uwepo wa kiwanda hiki ni jitihada za dhati za Rais Samia Suluhu Hassani kutengeneza ajira kwa Vijana wa kitanzania”
Kwa upande wake Mwekezaji wa kiwanda hicho Rashid Hamud (Liemba) amesema kiwanda hicho kitasimama endapo kitapata oda za kutosha na kitasaidia sana kuleta fedha za kigeni hapa nchini ambapo kitakapoanza uzalishaji Vijana zaidi ya 150 watapata ajira “Serikali itusaidie tupate oda nyingi tu”