Tume ya Uchaguzi nchini Nigeria (INEC) imeanza kutangaza matokeo ya majimbo kwa uchaguzi mkuu uliofanyika siku ya Jumapili, huku vyama vyote vikilalamikia mapungufu na ukiukwaji wa sheria na kanuni za uchaguzi.
Matokeo ya kwanza kutoka jimbo la Ekiki yalionesha kura nyingi zilikwenda kwa mgombea urais wa chama tawala (APC), Bwana Bola Tinubu, ambaye alijikusanyia kura 200,000 dhidi ya Atiku Abubakar wa chama kikuu cha upinzani cha PDP aliyepata chini ya nusu ya kura hizo, huku Peter Obi wa chama cha Labour akipata kura 11,000 japo bado vywma vyote vililamikia uwepo wa uiiukwaji wa sheria na kanunu katika uchaguzi huo.
Hata hivyo, matukio ya uvunjifu wa amani ywpishuhudiwa huku wanajeshi wakiwatia nguvuni watu 15 waliohusika na tukio hayo.
Kura za urais na ubunge hukusanywa kwenye kila jimbo kati ya majimbo 36 ya Nigeria kabla ya hesabu zake kupelekwa kwenye kituo kikuu cha majumuisho katika mji mkuu, Abuja.